Mwanamuziki R Kelly GerezaniMwanamuziki R Kelly Gerezani

R Kelly Akimbizwa Hospitalini, Azidishiwa Dawa Gerezani

R. Kelly, ameripotiwa kukimbizwa hospitali Ya ‘Duke University Mjini Durhan (North Calorina) baada ya kupoteza fahamu gerezani Butner, N.C, kutokana na kuzidishiwa dawa alizopewa na wahudumu wa afya wa gereza Hilo.

Afya ya muimbaji huyo imekuwa hatarini tangu aanze kifungo, chake akisumbuliwa na presha na kisukari. Hali hiyo imeibua hofu kwa miongoni mwa mawakili wake, wakidai kuwa kuna njama ya kumuua ikihusisha maafisa wa gereza, wakitoa ushahidi kutoka kwa mfungwa aliyedai kushawishiwa kumuua Kelly kwa ahadi ya kuachiwa huru. Hivyo Wameomba apewe kifungo cha nyumbani kutokana na hatari ya maisha yake gerezani.

Lakini Pia Kupitia Kipindi Cha ‘The Breakfast Club’ Waliwahi Kuripoti Kuwa #Rkelly Amekuwa Akiomba Msaada Wa Kimatibabu Ya Miguu Yake Ambayo Imevimba Pamoja Na Matatizo Ya Mapafu. Lakini Wanasheria Wake Wanadai Walikataliwa Ombi Hilo.

Kelly mwenye umri wa miaka 58, anatumikia kifungo cha miaka 30 kwa makosa ya unyanyasaji wa kingono N.k


Alikataa kuolewa ili amkomboe mama yake... Lakini mama ndiye aliyemuuza!

GORYANAH –Hii ni story ya Moto Sana yenye hisia na Mafunzo, binti jasiri anayepambana na siri nzito, umaskini na hatari kubwa kwa ndoto zake! Pakua app yetu ufurahie Sehemu ya 1 Hadi ya 5,na mwendelezo wake kila JUMAMOSI SAA MOJA KAMILI JIONI BURE!

BONYEZA HAPA KU DOWNLOAD.

Ukiona ujumbe wa allow notification bonyeza allow ili uwe mwanafamilia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *