Rais wa Cyril Ramaphosa Amkana Vikali Wicknell Chivayo, Adai Hamfahanu

Rais wa Cyril Ramaphosa Amkana Vikali Wicknell Chivayo, Adai Hamfahanu
Rais wa Cyril Ramaphosa Amkana Vikali Wicknell Chivayo, Adai Hamfahanu

Rais wa Cyril Ramaphosa amesema kuwa hamfahamu Mfanyabiashara wa Zimbabwe mwenye utata, Wicknell Chivayo, kufuatia uvumi ulioibuka kuhusu uhusiano wao wa karibu.

Kauli hiyo imekuja baada ya ziara ya Rais Ramaphosa tarehe 3 Mei 2026 katika shamba la Rais Emmerson Mnangagwa lililopo eneo la Kwekwe, katikati mwa Zimbabwe, ambapo walionekana wakikagua miradi ya kilimo ikiwemo mifugo, mazao ya nafaka, viazi na ufugaji wa samaki.

Wakati wa ziara hiyo, Chivayo mwenye umri wa miaka 43 alionekana karibu na viongozi hao wawili, jambo lililoibua maswali na uvumi mkubwa kuhusu nafasi yake na uhusiano wake na uongozi wa Afrika Kusini.

Chivayo amewahi kuhusishwa na zabuni mbalimbali zenye utata, zikiwemo za vifaa vya uchaguzi, usalama, miundombinu ya intaneti, umeme, huduma za afya za saratani.

Hata hivyo, Serikali ya Afrika Kusini haijatoa maelezo zaidi kuhusu uwepo wake katika ziara hiyo, huku mjadala ukiendelea katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu uhusiano wake na viongozi hao

Related Posts