Ronaldo na Mane Waangukia Pua Tena, Gamba Osaka FC Ikiitwaa Ubingwa AFC Champions League 2

Ronaldo na Mane Waangukia Pua Tena, Gamba Osaka FC Ikiitwaa Ubingwa AFC Champions League 2
Ronaldo na Mane Waangukia Pua Tena, Gamba Osaka FC Ikiitwaa Ubingwa AFC Champions League 2

Cristiano Ronaldo anaendelea kusuburi kubeba taji rasmi ndani ya klabu ya Al Nassr FC baada ya klabu hiyo kupoteza 1-0 kwenye fainali ya michuano ya ‘AFC Champions League two’ dhidi ya Gamba Osaka ya Japan katika dimba la Al Awwal Park, Riyadh, Saudi Arabia.

Gamba Osaka imetwaa ubingwa wa Kombe hilo kwa mara ya kwanza huku Ronaldo akiangukia pua kwa mara nyingine ingawa ana nafasi ya kumaliza msimu na Kombe kwani Al Nassr FC ipo kileleni mwa msimamo wa Saudi Pro League na inahitaji ushindi kwenye mchezo wa kufunga pazia la ligi hiyo ili kutwaa ubingwa.

FT: Al Nassr FC 🇸🇦 0-1 🇯🇵 Gamba Osaka
⚽ 30’ Hummet

Related Posts