
Depu Aiaga Yanga na Mashabiki, Akerjea Petro de Luanda ya Angola
Mshambuliaji wa kimataifa kutoka Angola, Laurindo Dilson ‘Depu’, amewaaga rasmi mashabiki wa klabu ya Yanga pamoja na Watanzania baada ya kukamilisha taratibu za kurejea nchini kwao kujiunga na miamba ya soka, Petro de Luanda.
Depu, aliyesajiliwa na Yanga mnamo Januari 2026 akitokea Radomiak Radom ya Poland, ametoa shukrani za dhati kwa mapokezi makubwa, upendo na ushirikiano aliopata kutoka kwa viongozi, wachezaji wenzake, na mashabiki katika kipindi chote alichohudumu klabuni hapo.
Katika ujumbe wake wa kuaga, Depu alisema: “Kila mmoja wenu atabaki kwenye kumbukumbu zangu. Ninajisikia mwenye bahati sana kwa kila kitu nilichopata. Hii si kwaheri, bali ni tutaonana hivi karibuni. Asanteni sana, Tanzania.”
Mshambuliaji huyo anarejea Petro de Luanda kuimarisha safu yao ya ushambuliaji kuelekea msimu ujao, huku akiacha alama ya ushirikiano wake wa muda mfupi ndani ya kikosi cha Wananchi.
