UWEZO WA DUKE ABUYA NA MANENO YA VICENTE DEL BOSQUE

Ndio nimeamka baada ya tafakuri nzima ya usiku wa jana baada ya Derby. Nilifanikiwa kuitazama kwa umakini, huku kiungo cha Yanga kikionyesha kuwa ‘Serious na kazi’

Tafakuri yangu ilinirudisha nyuma sana mpaka kwa kocha aliyewahi kufundisha Real Madrid na timu ya Taifa Spain wakati anaongelea ubora wa mtaalamu wa boli; Sergio Busquet, alisema kuwa “IF YOU WATCH THE GAME, YOU DON’T SEE BUSQUET. BUT IF YOU WATCH BUSQUETS, YOU SEE THE WHOLE GAME”

Alimaanisha kuwa, Ukiangalia mechi unaweza usimuone Busquet, ila ukimuangalia Busquet unaweza kuiona mechi nzima. Kimsingi, Vicente alikua anaonyesha ni kwa kiasi gani Barcelona ilikua inatakata dimbani kupitia Ubongo wa Sergio Busquet, ramani za ushindi, utulivu wa kiungo cha Barca ulikua chini ya nyayo za mtaalamu huyo.

Maneno ya Vicente Del Bosque yamenirudisha haraka kwenye Derby ya jana. Wakati wengi wenu mkisifia sana uwezo wa Pacome, kwangu mimi DUKE ABUYA alitembeza sana utakaso kwenye nyasi za Dimba la mkapa.

Ilikua ni ngumu kuelewa Yanga nzima nani ni bora nani kazingua ila ilikua pia ni rahisi zaidi kuielewa Yanga kupitia kumtazama Duke Abuya pekee yake ungeweza kuelewa ramani zote zilizokua zinachorwa dimbani kupitia Ubongo wake.

Tazama Utulivu wake, Unatia tick✅
Usahihi wake wa kupiga pass, tick✅
Ukabaji wake bila faulo, tick✅
Discipline ya eneo, tick✅

Okay, niliweza kuielewa Yanga kwa kumtazama Duke Abuya, kila kitu alichofanya kiligeuka kuwa dhahabu, alifanya kiungo cha Yanga kizibe mianya yote ya Simba kutawala, alileta utulivu wa timu kutengeneza mashambulizi, na pia aliunganisha vizuri build up phase ya Yanga na Attacking phase yao

Kama kuna mtu nimemkera kwa maneno yangu ya jioni ya leo naomba anisamehe, mimi nae ni binadamu


Alikataa kuolewa ili amkomboe mama yake... Lakini mama ndiye aliyemuuza!

GORYANAH –Hii ni story ya Moto Sana yenye hisia na Mafunzo, binti jasiri anayepambana na siri nzito, umaskini na hatari kubwa kwa ndoto zake! Pakua app yetu ufurahie Sehemu ya 1 Hadi ya 5,na mwendelezo wake kila JUMAMOSI SAA MOJA KAMILI JIONI BURE!

BONYEZA HAPA KU DOWNLOAD.

Ukiona ujumbe wa allow notification bonyeza allow ili uwe mwanafamilia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *