Simba Yaipiga Pamba Jiji 2-1 Mwanza, Yakwea Kileleni mwa Ligi Kuu

Simba Yaipiga Pamba Jiji 2-1 Mwanza, Yakwea Kileleni mwa Ligi Kuu
Simba Yaipiga Pamba Jiji 2-1 Mwanza, Yakwea Kileleni mwa Ligi Kuu

Simba Yaipiga Pamba Jiji 2-1 Mwanza, Yakwea Kileleni mwa Ligi Kuu

Klabu ya Simba SC imeendeleza mwanzo mzuri katika Ligi Kuu ya NBC (2026/27) baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Pamba Jiji FC kwenye Mchezo uliopigwa jijini Mwanza.

Wekundu wa Msimbazi walianza kupata mabao yao mapema kupitia kwa Clatous Chama katika dakika ya 18 na Oura dakika ya 30. Hata hivyo, Simba ilikumbana na mtihani mchezonapo baada ya kiungo Ibraheem Jabaar kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 44. Licha ya kucheza pungufu kwa kipindi chote cha pili, Simba ililinda ushindi wake ingawa Pamba Jiji ilipata bao la kufuta machozi kupitia kwa Diomande dakika ya 72.

Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha alama 6 baada ya mechi mbili na kupanda hadi kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu.

Related Posts