Spika wa Bunge la Tanzania Dkt. Tulia Ackson amewataka wabunge wanaoongea na simu bungeni kutoka nje ya ukumbi wa bunge kwani wanatumia sauti kubwa ambayo inaondoa utulivu katika vikao vya bunge.
Dkt. Tulia alifafanua kuwa anafahamu kuwa kuna wabunge wanakabiliwa na usumbufu wa wajumbe majimboni na amewasisitiza kuwa kama wanahitaji kuzungumza vizuri, ni bora waende nje ya ukumbi wa bunge.
“Wale mnaoongea na simu mnaanza kidogo kidogo lakini baadae sauti zinapanda sijui wajumbe wanawasumbua huko lakini waheshimiwa wabunge ambao ni lazima mzungumze na simu naomba muende nje” Dkt. Tulia Ackson – Spika wa Bunge la Tanzania
Agizo hili lina lengo la kuboresha mazingira ya utulivu na ufuatuliaji wa kikao cha bunge kinachoendelea ili wabunge waweze kuzingatia mjadala unaoendelea wa Hali ya Uchumi wa Taifa na Bajeti kuu ya serikali.

