Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amemshukuru Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini mara mbili ikiwemo kumpa nafasi ya kuwa Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na baadaye Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambapo Makonda amesema licha ya baadhi ya Watu kumkandamiza kisa mapambano yake ya kupinga dawa za kulevya na ushoga lakini bado haikumzuia Rais Samia kumuamini na kumpa fursa.
Akiongea leo June 24, 2025, kwenye Jukwaa la Wanawake lililofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano (AICC) Jijini Arusha, Makonda amesema “Mh. Mgeni rasmi Balozi (Dkt. Nchimbi), naomba kwa unyenyekevu mkubwa unifikishie salamu kwa Rais Samia kwa kuniamini mara mbili ndani ya utumishi wake wa urais tangu mwaka 2021, kuniteua kuwa Msemaji wa Chama Cha Mapinduzi na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, sikutarajia leo itakuwa hotuba yangu ya kuaga”
Alikataa kuolewa ili amkomboe mama yake... Lakini mama ndiye aliyemuuza!
GORYANAH –Hii ni story ya Moto Sana yenye hisia na Mafunzo, binti jasiri anayepambana na siri nzito, umaskini na hatari kubwa kwa ndoto zake! Pakua app yetu ufurahie Sehemu ya 1 Hadi ya 5,na mwendelezo wake kila JUMAMOSI SAA MOJA KAMILI JIONI BURE!
Ukiona ujumbe wa allow notification bonyeza allow ili uwe mwanafamilia.