TANZIA: Mtangazaji Ssebo wa EFM na TVE Afariki Dunia

  TANZIA: Mtangazaji Ssebo wa EFM na TVE Afariki Dunia
TANZIA: Mtangazaji Ssebo wa EFM na TVE Afariki Dunia

Usiku wa kuamkia leo, Jumatano Machi 11.2026, Tasnia ya Habari imepokea taarifa ya masikitiko kufuatia kifo cha mmoja wa Viongozi Waandamizi wa EFM na TVE Denis Busulwa (Ssebo)

Taarifa za msiba Ssebo ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Uendeshaji na Biashara wa EFM na TVE zimetengazwa na Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa vyombo hivyo vya Habari Antony Ciza Majey (Majizzo) kupitia chapisho lake aliloweka kwenye mtandao wake binafsi wa Instagram ambapo ameeleza kuwa kifo hicho kimetokea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar es Salaam

Kupitia chapisho hilo, Majizzo amemuelezea Ssebo kuwa ni mtu aliyekuwa nguzo muhimu kwenye maisha yake, sio tu kwa sababu alikuwa Kiongozi mwenzake ndani ya EFM na TVE bali pia kwake alikuwa rafiki, kaka na ndiye aliyekuwa Msimamizi wa ndoa yake,

Amesema enzi za uhai wake Marehemu Ssebo ameitumikia EFM na TVE kwa nguvu zake zote, na kwa sasa taratibu za mazishi zinaendelea na taarifa zaidi zitatolewa hapo baadae

Related Posts