Nature

TRUMP: Elon Musk Asepe tu Simuhitaji Tena

TRUMP: Elon Musk Asepe tu Simuhitaji Tena

Rais wa Marekani, Donald Trump, ametangaza kuwa uhusiano wake na mfanyabiashara bilionea Elon Musk umekwisha rasmi, akisisitiza kuwa hana mpango wa kurekebisha uhusiano huo uliokuwa wa karibu hapo awali.

“Ninadhani hivyo,” Trump aliiambia NBC News alipoulizwa iwapo uhusiano wao sasa umevunjika. Alijibu kwa “Hapana” alipoulizwa kama angependa kurejesha mahusiano hayo.

Kauli hiyo imekuja baada ya wiki kadhaa za mvutano wa wazi kati ya Trump na Musk, ambao hapo awali walishirikiana kwa karibu kisiasa na kibiashara, huku Musk akiwa miongoni mwa wafadhili wa kampeni ya Trump na mshauri wa sera katika Ikulu.

Chanzo kikuu cha mvutano huo ni muswada wa matumizi ya serikali, uliobatizwa jina la “Big Beautiful Bill”, ambao Musk amekuwa akiupinga vikali, akisema utaongeza mzigo mkubwa wa deni kwa taifa.

Musk aliandika kwenye mtandao wake wa kijamii X (zamani Twitter) kuwa muswada huo ni “chukizo”, japo hakumtaja Trump moja kwa moja. Alisisitiza kuwa muswada huo utadhoofisha juhudi za kubana matumizi serikalini, juhudi ambazo aliziongoza akiwa mkuu wa Idara ya Ufanisi wa Serikali (Doge) kabla ya kujiuzulu baada ya siku 129 tu kazini.

Mvutano ulizidi kuwa mkali pale Trump aliposema alikuwa “amesikitishwa” na tabia ya Musk, hali iliyomfanya Musk kumjibu kwa mfululizo wa chapisho kwenye X, akidai kuwa Trump asingeshinda uchaguzi bila msaada wake. Pia alimshutumu Trump kwa kuhusishwa na Jeffrey Epstein, mfadhili aliyekumbwa na kashfa ya biashara ya ngono kabla ya kufariki gerezani.

Trump hakukaa kimya. Kupitia mtandao wake wa Truth Social, alimuita Musk “mwendawazimu”, na kutishia kukata kandarasi zote za biashara kati ya Musk na serikali ya shirikisho.

Katika mahojiano hayo ya NBC News, Trump aliongeza kuwa Musk hana heshima kwa ofisi ya rais, akisisitiza kuwa hali ya sasa ni kinyume na ushirikiano wao wa zamani.

ALSO READ | EDO Kumwembe: FEISAL Salum Atafika Akiwa Hoi Saana

Related Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *