Uchaguzi Mkuu Yanga 2026: Eng. Hersi Said na Arafat Haji Waongezewa Miaka Minne

Wanachama wa Klabu ya Yanga SC wameipitisha tena safu ya uongozi wa juu ya klabu hiyo kufuatia Uchaguzi Mkuu uliofanyika Agosti 2, 2026, kwa kumchagua Eng. Hersi Said kuendelea kuwa Rais na Arafat Haji kuwa Makamu wa Rais kwa muhula mwingine wa miaka minne.

Akihutubia wanachama, Eng. Hersi aliorodhesha mafanikio makubwa ya utawala wake katika miaka minne iliyopita, akibainisha kuwa kwenye Ligi Kuu ya NBC, Yanga ilicheza mechi 120, ikishinda 101, sare 12, na kupoteza mechi 7 pekee—huku ikikusanya pointi 315 na kufunga mabao 286.

Dominance ya Ndani na Nje ya Nchi:

Mbali na kutwaa Kombe la Shirikisho la CRDB mara nne mfululizo bila kupoteza mchezo katika mechi 28, Yanga imetwaa Ngao ya Jamii mara 4 pamoja na mataji ya kimataifa ya kirafiki kama Toyota Cup (Afrika Kusini) na Rayon Day Cup (Rwanda). Hersi aliwashukuru viongozi waliomaliza muda wao na kuahidi kushirikiana na viongozi wapya watakaochaguliwa kwa ajili ya ustawi wa Wananchi.

Related Posts