Ahmed AllyAhmed Ally

Waliokata Ticket Simba Vs Berkane Kwa Mkapa Wapewa Muongozo Huu Mpya

Klabu ya Simba Sc imewataka mashabiki wake walionunua tiketi kwa ajili ya mchezo wa fainali ya kombe la Shirikisho Afrika katika ambao awali ilidhaniwa ungechezwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa wazitunze tiketi hizo kwa ajili ya kuzitumia kwenye Simba Day.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ahmed Ally ametangaza utaratibu mpya wa viingilio kuelekea mchezo huo ambao sasa utachezwa katika dimba New Amaan, Complex Zanzibar.

Simba SC imetangaza utaratibu mpya wa kukata tiketi na kutangaza bei mpya za viingilio ambavyo ni

VIP A – Tsh 50,000
Urusi – Tsh 30,000
Mzunguko- Tsh 10,000

Simba imeongezea kuwa waliokata tiketi awali ambapo uwanja ulikuwa Benjamin Mkapa , watunze tiketi hizo zitatumika Simba Day mwezi Agosti

“Mchakato wa uuzwaji wa Tiketi umeanza upya, hivyo wale wote ambao mlinunua Tiketi zitunzeni mtazitumia siku ya Simba Day._ Kauli ya Afisa Habari wa Simba Ahmed Ally akizungumza na wanahabari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *