Yanga Yatupwa Nje ya Mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika Licha ya Kumtandika Mwarabu

Shughuli ya imemalizika katika dimba la New Amaan Complex, Zanzibar huku wananchi, Young Africans Sc wakisukumizwa nje ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) baada ya Al Ahly kutoshana nguvu na AS Far Rabat kwa sare tasa licha ya Yanga Sc kushinda kwa kishindo.

AS Far Rabat wameungana na Al Ahly kwenye robo fainali ya michuano hiyo huku Yanga Sc ikiungana na Simba Sc, Azam FC na Singida Black Stars kurudi nyumbani baada ya timu zote kutoka Tanzania kuaga michuano ya CAF msimu huu.

FT: Yanga Sc 🇹🇿 3-0 🇩🇿 JS Kabylie
⚽ 36’ Depu
⚽ 63’ Depu
⚽ 66’ Boka

FT: Al Ahly 🇪🇬 0-0 🇲🇦 FAR Rabat

MSIMAMO KUNDI B kwenye mabano (magoli ya kufunga na magoli ya kufungwa)
1.🇪🇬 Al Ahly – pointi 10 (8-3)
2.🇲🇦 FAR Rabat – pointi 9 (3-2)
3.🇹🇿 Yanga Sc – pointi 8 (5-4)
4.🇩🇿 JS Kabylie – pointi 3 (1-8)

Related Posts