Mzee Butiku ‘Sijui Pole Pole Alipo ila Niliongea Naye’

Baada ya uwepo wa minong’ono ya muda mrefu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mwalimu Nyerere Foundation Mzee Joseph Waryoba Butiku pengine anafahamu alipo au anajuwa kuhusu kilichompata aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania kwenye nchi za Malawi na Cuba Humphrey Polepole leo, Jumatatu Januari 19.2026 Mzee huyo amejitokeza na kukanusha madai hayo

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mzee Butiku amesema hafahamu alipo Polepole ingawa awali alizungumzanae karibu mara tatu kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo suala la Uchaguzi Mkuu na dhamira yake ya kujiuzulu Ubalozi

Related Posts