Klabu ya Al-Ittihad SC ya Libya imekamilisha rasmi usajili wa kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki kutoka Wydad Athletic Club baada ya kuinunua mkataba wake kwa kiasi cha USD 500,000 (takribani Tsh bilioni 1.2).
Kwa kukamilika kwa dili hilo, Stephane Aziz Ki sasa ni mali halali ya Al-Ittihad SC, hatua inayoongeza nguvu kubwa katika safu ya kiungo ya klabu hiyo.
Usajili huo unaashiria dhamira ya Al-Ittihad SC kuwekeza kwa wachezaji wenye ubora na uzoefu wa juu.
