Mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu Tanzania Bara klabu ya Yanga Sc imetoa taarifa njema na nzito kwa mashabiki wa soka nchini Tanzania haswa wa klabu hiyo kuhusiana na mshambulianji wao tegemezi wa sasa anayejulikana kwa jina la Depu.
Klabu ya Yanga Sc imemchagua Depu kuwa ndiye mchezaji wao bora wa mwezi wa Januari na hii inatokana na ubora na kiwango kikubwa alichokionyesha mchezaji huyo kwenye mechi mbili za Nbc Premier league ambazo amecheza akiwa na jezi ya Yanga Sc ndani ya mwezi Januari.
Taarifa ya Depu kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa klabu ya Yanga Sc ndani ya mwezi Januari imetolewa na klabu hiyo kupitia kwenye ukurasa wa Instagram wa Instagram wa timu hiyo ikiwa ni masaa machache kabla ya Yanga Sc kuvaana na FAR Rabat kwenye mchezo wa marudiano wa hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika.
Depu ameshinda tuzo hiyo kutokana na takwimu zake zinaonyesha kwamba ndani ya mwezi Januari akiwa na kikosi cha Yanga Sc, amecheza mechi mbili za Nbc Premier league na amefanikiwa kufunga jumla ya magoli 3 kitu ambacho ni kikubwa sana ukilinganisha na takwimu za mastaa wengine wa klabu hiyo.
Tuzo hii aliyopewa Depu kwa kiasi kikubwa inaenda kumuongezea morali kubwa sana kuelekea kwenye mchezo ujao ambao atavaana na wababe wa soka la nchini Morocco klabu ya FAR Rabat kwenye hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika.
Je, wewe kama mdau na shabiki wa soka la Tanzania bara unatoa maoni gani kuhusiana na tuzo hii iliyotolewa na Yanga Sc kwenda kwa Depu?.
Chanzo: ukurasa wa Instagram wa klabu ya Yanga Sc
