Wekundu wa Msimbazi, Simba Sc wamesukumizwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL kufuatia sare ya 1-1 dhidi ya Petro De Luanda ya Angola kwenye mchezo wa kundi D.
Simba Sc imefikisha alama mbili tu baada ya mechi tano kwenye kundi hilo huku wakisaliwa na mchezo mmoja wa kukamilisha ratiba.
Petro De Luanda 🇦🇴 1-1 🇹🇿 Simba Sc
⚽ 13’ Pinto
♦️ 39’ Kapombe
⚽ 81’ Oura
MSIMAMO KUNDI D
1. Stade Malien – mechi 4 – pointi 8
2. Esperance – mechi 4 – pointi 6
3. Petro Luanda – mechi 5 – pointi 6
4. Simba Sc- mechi 5 – pointi 2
