Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa onyo rasmi na kupiga marufuku matumizi ya noti za shilingi za Kitanzania (TZS) kutengeneza mashada ya maua (cash bouquets), mapambo au garlands za maua na vitu vingine vya sherehe kuelekea msimu wa Valentine
Gavana wa benki hiyo, Emmanuel Tutuba, amesema kitendo hicho ni uharibifu wa fedha za taifa (defacement of currency) na ni kinyume cha sheria na kubainisha kwamba watakaobainika kutenda kosa hilo wanaweza kukabiliwa na adhabu ya faini ya hadi Shilingi Milioni tano.
Sababu ya marufuku hiyo ni kwamba kukunja, kubandika, kushona au kuweka noti hivyo huharibu ubora wake, hivyo haziwezi kutumika tena vizuri kwenye ATM, mashine za kuhesabu fedha au mzunguko wa kawaida, hali inayoleta gharama kubwa kwa taifa kuchapa noti mpya mara kwa mara.
