
Kiungo Mshambuliaji wa Kimataifa wa Burkina Faso 🇧🇫, Stephanie Aziz Ki amewasili nchini Tanzania hii leo na kuelekea Jijini Dodoma ambako alialikwa na Waziri wa Madini ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Klabu ya Yanga SC, Antony Mavunde.
Aziz Ki ni miongoni mwa wageni waalikwa waliokuwepo leo kwenye uzinduzi wa Michuano ya Ujirani Mwema Cup inayofanyika Jijini Dodoma amnapo Mhe Mavunde na Aziz Ki wamepata nafasi ya kutembelea Kijiji cha Matumaini kilichopo Kisasa Jijini,Dodoma kuwaona watoto yatima na kutumia nafasi hiyo pia kutoa sadaka yao kwa ajili ya watoto hao.
Pia wametembelea Hospital ya Rufaa ya Mkoa kuangalia jengo la mapumziko la wananchi wanaokuja kuwaangalia wagonjwa wao ambalo Aziz Ki na Djigui Diarra walichangia kulijenga kwa kuchangia mifuko ya saruji.
