Yanga Waichapa Namungo Kwa Mbinde, Haya Ndio Yaliyojiri

Yanga Waichapa Namungo Kwa Mbinde, Haya Ndio Yaliyojiri
Yanga Waichapa Namungo Kwa Mbinde, Haya Ndio Yaliyojiri

Dakika 25 za kwanza timu zote mbili hazikuwa na umiliki mzuri wa mchezo , hakuna usahihi wa pasi , wanatupa mipira kirahisi sana ( hakuna game management ) .

✍🏼 Yanga na muundo wao kama kawaida wakiwa na mali 2-1 then FBs wao wanakuwa pembeni zaidi ya kiwanjani dhumuni ni kuongeza machaguo ya pasi zao na kuwafanya Namungo kuzuia eneo kubwa la uwanja na walifanikiwa .

✍🏼 Uwepo wa Maxi na Duke kama namba 8 wawili au 10 wawili ilitoa msingi sahihi kwa Yanga kuunganisha pasi zao vizuri tatizo likawa ni nini ?

A) Hakuna mchezaji mwenye uwezo wa kutengeneza nafasi eneo la mwisho badala yake wakawa wanatumia mawinga wao kushambulia β€œ Half Spaces β€œ kuifungua Namungo .

B) Namungo bila mpira wanakuwa na wachezaji wengi eneo la nyuma , maana yake Yanga wanatakiwa kuwa na mchezaji mwenye uwezo wa kupasia mpira vizuri kwenda mbele ( walikosa mtu kama huyo ) .

✍🏼 Nafikiri kocha wa Namungo β€œ Juma Mgunda β€œ alijua kabisa hawezi kupishana na Yanga , alichokifanya ni kuzuia na idadi kubwa ya wachezaji then wanashambulia kwa kushtukiza . ( waliongeza Utulivu , usahihi wa pasi zao na uthubutu wa kushambulia nafasi eneo la mbele ) Kuna nyakati quality ndio iliwaangusha na idadi ndogo ya wachezaji eneo la mbele .

NOTE :

1: DEPU anafunga goli lake la nne ndani ya NBCPL : amefunga kwenye kila mchezo .

2: Ile ya Maxi ni Clear Penalty βœ… Namungo walistahili kupewa tuta .

3: Okello anatakiwa kuboresha game yake ( mipira inapoteza kirahisi sana ) .

4: Maxi Nzegeli , Duke Abuya na Camara wametengeneza muunganiko mzuri kwenye kiungo ( timu ikiwa na mpira na bila mpira ) .

5: Job na Bacca ameshinda mipambano yao vizuri sana πŸ‘πŸ½

FT : Namungo 0-1 Yanga Sc

By Kelvin Rabson

Related Posts