![]()
Iran imemchagua Ayatollah Mojtaba Khamenei kuwa Kiongozi Mkuu wa Taifa hilo kufuatia kifo Ayatollah Ali Khamenei ambaye alikuwa baba yake, aliyeuawa Februari 28, 2026 kufuatilia mashambulizi ya mabomu yaliyofanywa na Marekani ikishirikana na Israel.
Jina la Ayatollah Mojtaba ambaye ni mtoto wa pili wa kiume wa Khamenei limetangazwa na televisheni ya taifa baada ya kuwa limepitishwa na Baraza maalum la Wataalamu linalohusika na kuchagua Kiongozi Mkuu wa taifa hilo.
Mojtaba mwenye umri wa miaka 56 anachukua utawala wa Iran katika wakati mgumu wa vita kutoka kwa baba yake ambaye aliliongoza taifa hilo kwa miaka takribani 37.
Aidha utawala wake unakabiliwa na na upinzani mkali kutoka kwa Marekani na Israel ambao wanaendelea kuishambulia Iran huku wakidai kuwa mtawala mpya wa Iran lazima wamuue.
Ikumbukwe Rais wa Marekani Donald Trump wakati wamemuua Khamenei aliwataka wananchi wa Iran kuungana nae kuuondoa uongozi uliopo. Baadae Trump alipigilia msumari ajenda yake kwa kusema kuwa “mtawala mpya wa Iran hatadumu kama Marekani haikushirikishwa katika uchaguzi wake”. Huku Israel ikiahidi “kumuwinda na kumuua” mtawala mpya.
Wachambuzi wa kisiasa wanaeleza kuwa endapo vita vikiisha kwa Iran kushinda na Mojtaba akawa hai basi anaweza kuwa kiongozi mwenye nguvu zaidi katika Mashariki ya kati lakini pia mwenye ushawishi zaidi Iran.
