
Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema kuwa vita vinavyoendelea katika eneo la Mashariki ya Kati vinatarajiwa kumalizika hivi karibuni.
Kauli hiyo aliitoa wakati akijibu swali la mwandishi wa habari aliyemuuliza ni muda gani operesheni ya kijeshi ya Marekani inayofanyika nchini Iran itachukua hadi kukamilika.
Akijibu swali hilo, Trump alisema anaamini operesheni hiyo haitachukua muda mrefu kumalizika, ingawa alibainisha kuwa haitakamilika ndani ya wiki hii.
“Nafikiri itamalizika hivi karibuni. Kila kitu ambacho Iran ilikuwa nacho kimeharibiwa, ikiwa ni pamoja na uongozi wao,” alisema Trump.
Aidha, Trump alidai kuwa hata kiongozi anayetajwa kuchukua nafasi ya kiongozi mkuu wa kidini wa Iran, Ali Khamenei, bado hafahamiki sana kwa wananchi wengi.
“Watu wengi hata hawajasikia kuhusu kiongozi wanayemzungumzia kuchukua nafasi ya ayatollah,” aliongeza rais huyo wa Marekani.
