TANZIA: Waziri William Lukuvi Afariki Dunia

TANZIA: Waziri William Lukuvi Afariki Dunia
TANZIA: Waziri William Lukuvi Afariki Dunia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametangaza kifo cha mwanasiasa mbobezi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), William Vangimembe Lukuvi.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa leo, Jumatano, Machi 25, 2026, na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses M. Kusiluka, Lukuvi amefariki dunia majira ya saa moja asubuhi katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa Lukuvi alikuwa akipatiwa matibabu katika hospitali hiyo kufuatia ugonjwa wa mshtuko wa moyo uliomfika ghafla. Lukuvi amefariki akiwa bado anatumikia nafasi yake kama Mbunge wa Jimbo la Isimani na Waziri katika Baraza la Mawaziri la Rais Samia.

Rais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, familia ya marehemu, wananchi wa Jimbo la Isimani, pamoja na ndugu, jamaa, na Watanzania wote waliofikiwa na msiba huu mzito.

Related Posts