
Serikali ya Uganda imetangaza rasmi kuondolewa kwa ada ya viza kwa wageni wakati wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.
Hatua hii ya kimkakati inalenga kurahisisha uingiaji kwa Mashabiki na watalii na kurahisisha katika kukuza uchumi wa nchi.
Mpango huo ni sehemu ya juhudi pana za kufufua sekta ya utalii ya nchi.
Uganda inatarajia kuongezeka kiuchumi na kutoa fursa ya kipekee kwa Watalii na wageni wakati wa Mashindano hayo makubwa barani Afrika.
