Papa Amjibu Vikali Trump Baada ya Kauli Zake, Asema Haogopi Vitisho

Papa Amjibu Vikali Trump Baada ya Kauli Zake, Asema Haogopi Vitisho
Papa Amjibu Vikali Trump Baada ya Kauli Zake, Asema Haogopi Vitisho

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Pope Leo XIV, amemjibu vikali Rais wa Marekani Donald Trump kufuatia kauli kali zilizotolewa dhidi yake kwenye mitandao ya kijamii, akisisitiza kuwa haogopi shinikizo lolote la kisiasa.

Akizungumza na waandishi wa habari akiwa ndani ya ndege ya kipapa akiwa safarini kuelekea Algeria, Papa Leo alisema wazi kuwa hana hofu na utawala wa Marekani na ataendelea kusimamia ujumbe wa Kanisa.

“Nina uhuru kamili na sina hofu yoyote ya utawala wa Trump au kuzungumza kwa sauti kuhusu ujumbe wa Injili, ambao ndio ninauamini kuwa ndio wajibu wangu,” alisema Papa.

Ndege iliyombeba Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo XIV, pamoja na ujumbe wake, imeondoka asubuhi ya leo, April 13, 2026 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Roma-Fiumicino kuelekea katika ziara yake ya tatu ya kimataifa ya kitume barani Afrika.
Kauli hiyo imekuja baada ya Trump kumshambulia Papa kupitia mtandao wake wa Truth Social, akimkosoa kwa kile alichokiita misimamo ya “kiliberali” katika masuala ya uhalifu na sera za kimataifa.

Trump alimuita Papa “dhaifu katika masuala ya uhalifu” na “asiyefaa katika sera za nje,” kauli ambazo zimezua mjadala mpana kimataifa.

Papa Leo, hata hivyo, alisisitiza kuwa yeye na Kanisa Katoliki si wanasiasa na hawashughulikii sera za kimataifa kwa mtazamo wa kisiasa kama serikali zinavyofanya.

“Sisi si wanasiasa. Tunafuata ujumbe wa Injili na kuwa wajumbe wa amani,” aliongeza.

Mvutano huo unaendelea kuvuta hisia duniani, ukionyesha mgongano wa mitazamo kati ya uongozi wa kidini na kisiasa kuhusu masuala ya maadili, uongozi na sera za kimataifa.

 

Related Posts