Aua watoto wake 7 kwa risasi kisa ugomvi wa familia


Mtu mmoja amewaua watoto wake saba pamoja na mtoto mwingine asiye wa familia hiyo katika tukio la mauaji ya risasi lililotokea Shreveport, katika Jimbo la Louisiana nchini Marekani, huku polisi wakieleza tukio hilo kuwa ni mzozo wa kifamilia.

Kwa mujibu wa taarifa, watoto hao walikuwa na umri wa kati ya mwaka mmoja hadi miaka 14. Tukio hilo lilitokea majira ya saa 5:00 asubuhi, ambapo mshukiwa alipiga risasi watu 10 kabla ya kukimbia kwa kutumia gari lililoibiwa.

Msemaji wa Polisi wa Shreveport, Chris Bordelon, amesema polisi walimfukuza mshukiwa huyo na hatimaye kumuua.

Wanawake wawili watu wazima, akiwemo mama wa watoto hao, wamelazwa hospitalini wakiwa katika hali mahututi.

Mshukiwa ametambuliwa kama Shamar Elkins, kwa mujibu wa ofisi ya mawasiliano ya meya wa jiji hilo

Related Posts