Ikulu ya Nigeria Yakanusha Uvumi Kuhusu Mabadiliko ya Jina la Nchi

Ikulu ya Nigeria Yakanusha Uvumi Kuhusu Mabadiliko ya Jina la Nchi
Ikulu ya Nigeria Yakanusha Uvumi Kuhusu Mabadiliko ya Jina la Nchi

Ikulu ya Nigeria imekanusha taarifa zilizosambaa mitandaoni zikidai kuwa Rais Bola Tinubu anapanga kupendekeza marekebisho ya Katiba yatakayobadilisha jina la nchi hiyo kuwa Marekani ya Nigeria pamoja na kuondoa Sheria katika eneo la Kaskazini.

Katika taarifa iliyotolewa Alhamisi, ikulu hiyo imesema taarifa hizo ni za uongo na zinazopotosha umma, zikisisitiza kuwa zimebuniwa na watu wanaolenga kuchochea taharuki, mgawanyiko wa kisiasa na kuyumbisha taifa kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Ikulu imeongeza kuwa lengo la uvumi huo ni kuleta machafuko ya kisiasa na kupunguza imani ya wananchi kwa serikali katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa Januari 2027.

Nigeria inajiandaa kwa uchaguzi mkuu huo huku mjadala wa kisiasa ukiendelea kuwa mkali kuhusu mustakabali wa nchi hiyo yenye watu wengi zaidi barani Afrika.

Related Posts