Mchungaji Msigwa Ajiondoa CCM na Kurudi Chadema

Aliyekuwa mwanachama wa CCM, Peter Msigwa, ametangaza kujiondoa rasmi ndani ya chama hicho na kurejea CHADEMA baada ya kutafakari kwa kina kuhusu matukio ya ukiukwaji wa haki na utu wa binadamu yaliyotokea Oktoba 29, 2025.

Katika taarifa yake, Msigwa amesema hawezi kuendelea kuishi katika huzuni na ukimya kutokana na yaliyotokea, hivyo ameamua kurejea CHADEMA kwa kufuata taratibu zote za chama hicho.

Pia ameomba radhi kwa Watanzania na wanachama wa CHADEMA walioumizwa au kukatishwa tamaa na msimamo wake wa awali, akisema binadamu hukosea lakini dhamira inapozinduka ni muhimu kusimama upande wa haki, utu na demokrasia ya kweli.

Related Posts