
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu amerudi katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masijala Ndogo ya Dar es salaam kuomba kujumuishwa katika kesi ya madai ya mgawanyo usio sawa wa rasilimali ndani ya chama hicho kati ya Tanzania Bara na Zanzibar.
Hii ni mara ya pili kwa Lissu kufungua maombi hayo baada ya Mahakama kuyakataa maombi yake ya awali kwa sababu hakuweza kuonesha maslahi ya karibu katika kesi hiyo.
Kesi hiyo ya madai namba 8323 ya mwaka 2025 ilifunguliwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Said Issa Mohamed pamoja na Wajumbe wawili wa Bodi ya Wadhamini wa CHADEMA kutoka Zanzibar, Ahmed Rashid Khamis na Maulida Anna Komu ambaye ni marehemu.
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masijala Ndogo ya Dar es salaam imepanga kusikiliza maombi ya Mwenyekiti wa (CHADEMA) Tundu Lissu ya kutaka kujumuishwa katika kesi ya mgawanyo usio sawa wa rasilimali kati ya Tanzania Bara na Zanzibar, Juni 2, 2026.
Akizungumza na Waandishi wa Habari nje ya Mahakama hiyo, Wakili Dkt. Rugemeleza Nshala amesema, kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa baada ya kupokea wito wa Mahakama, Jaji ametusikiliza na kisha kutoa maelekezo kuwa tujibu maombi ndani ya siku saba”. Dkt, Nshala.
Aidha, katika kesi hiyo ambayo Lissu ameomba kujumuishwa kwa mara ya pili baada ya awali kukatiliwa maombi yake ilifunguliwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti, Said Issa Mohamed na wajumbe wawili wa Bodi ya Wadhamini wa CHADEMA kutoka Zanzibar, Ahmed Rashid Khamis na Maulida Anna Komu (marehemu).
