
Mume wa mwanamama Zari The Bosslady (45), kijana Shakib Cham (34), ameachia ujumbe mzito na wa dhati wa mapenzi kwenda kwa mkewe, unaothibitisha kuwa penzi lao bado linafukuta moto moto.
Katika ujumbe huo, Shakib ameandika:
“Mwaka mwingine tena nikiwa pamoja na wewe, na bado mimi ndiye mwanaume mwenye bahati zaidi duniani. Wewe ni nyumba yangu, utulivu mkuu wa moyo wangu, na mtu ninayempenda zaidi katika kila hatua ya maisha yangu.”
Licha ya utofauti wa umri kati yao, wawili hawa wanaendelea kuwathibitishia walimwengu kuwa umri ni namba tu pale mioyo inayopendana inapokutana. Umeupokeaje ujumbe huu wa Shakib?
