Yanga Wamejichanganya Kwenye Dili la Aziz Ki

Yanga Wamejichanganya Kwenye Dili la Aziz Ki
Yanga Wamejichanganya Kwenye Dili la Aziz Ki

Inawezekana tunaendelea kuendekeza sajili za kisiasa lakini Usajili wa Aziz Ki si usajili sahihi kwa Yanga. Najua sitaeleweka lakini huu ndio uhalisia ninaouona…

Aziz Ki ana umri wa miaka 31, Yanga wanataka kuwafurahisha mashabiki kwa kumrudisha kwa zaidi ya Bilioni 1 ili kukamilisha usajili huu. Watatakiwa kuvunja mkataba na kulipa Sign-on fee then kumlipa mshahara wa zaidi ya Milioni 50…

Huu ni uvivu mkubwa wa kufanya scouting, wakati ambao unaangaika kumsajili Aziz ambaye ni maji ya jioni ungeweza kuwapata wachezaji watatu wenye quality, umri unaruhusu hata kuwauza baadae, wenye njaa ya mafanikio na unawaoata kwa gharama ya kawaida…

Leo kwa sababu ni mwaka wa Uchaguzi watu wanatafuta Sympathy ya Umma wanaanza kurudi kule kwenye janjajanja. Ukweli ni kwamba hakuna namna Yanga inaweza kurudi kwenye ubora kwa short cut…

Jenga msingi kwanza acheni kuadaa watu…

GENZ INK…

Related Posts