
Yanga ana alama 69 baada ya kucheza mechi 28. Anahitaji alama 4 tu katika mechi mbili zilizobaki ili kumaliza ligi akiwa bingwa.
Alama hizo 4 zitamfikisha alama 73. Hata Simba akishinda mechi zake zote mbili, atafikisha alama 73 pia.
Ili Simba awe bingwa katika mazingira hayo, atalazimika kufunga zaidi ya mabao 14 katika mechi mbili zilizobaki dhidi ya Singida BS na KMC. ππππ
Tafsiri yake ni kwamba Yanga akishinda leo, atahitaji sare tu katika mchezo dhidi ya JKT Tanzania ili kuhitimisha safari yake ya kutwaa ubingwa kwa mara ya tano mfululizo.
Kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2004, ilipoanza kuitwa Ligi Kuu Bara, Yanga inakaribia kutwaa ubingwa kwa mara ya tano mfululizo baada ya kuupoka utawala wa Simba kwenye ligi mwaka 2022.
Simba ilitwaa ubingwa mara nne mfululizo kuanzia mwaka 2018 hadi 2021. Kabla ya hapo, Yanga ilitwaa ubingwa mara tatu mfululizo kuanzia mwaka 2015 hadi 2017.
Kutawala ligi kwa mara tano mfululizo ni jambo geni katika miaka ya hivi karibuni.
Yanga wana mechi mbili tu za kujitetea wenyewe na kuweka rekodi nyingine ngumu, baada ya kuweka rekodi ya unbeaten ndefu zaidi.
βοΈKALAMU YA USHAHIDI
@cheyolutenganotz
