SHTUKIZO LA KOMBE LA DUNIA: Ujerumani Nje, Paraguay Yasonga Mbele!

Germany Vs Paraguay
Germany Vs Paraguay

SHTUKIZO LA KOMBE LA DUNIA: Ujerumani Nje, Paraguay Yasonga Mbele!

Mabingwa mara nne wa kihistoria wa Kombe la Dunia, Ujerumani, wamefungashiwa virago vyao mapema kwenye michuano ya Kombe la Dunia la FIFA 2026. Hii ni baada ya kukubali kichapo cha penalti 4-3 dhidi ya Paraguay katika mtanange wa kukata na shoka wa hatua ya 32 bora.

Dakika 90 pamoja na muda wa nyongeza (Extra Time) zilimalizika kwa timu hizo kutosana nguvu ya 1-1, kabla ya Paraguay kuonyesha umahiri mkubwa kwenye matuta na kukata tiketi ya kusonga mbele.

Nini Kinafuata kwa Paraguay?

Kwa ushindi huo, Paraguay inafuzu rasmi hatua ya 16 bora, ambapo sasa itasubiri mshindi wa mechi nyingine kali ya hatua hii kati ya Ufaransa na Sweden ili kujua itacheza na nani.

Dondoo za Mchezo

Muda wa Kawaida na Nyongeza (FT & ET): Ujerumani 1-1 Paraguay Matokeo ya Penalti: Ujerumani 3-4 Paraguay

Wafungaji wa Mabao:

  • Paraguay 🇵🇾: Julio Enciso (Dakika ya 29)

  • Ujerumani 🇩🇪: Kai Havertz (Dakika ya 54)

Related Posts