
KISHINDO CHA ATLAS: Morocco Yaing’oa Uholanzi na Kutinga 16 Bora!
Simba wa Milima ya Atlas wameendeleza ubabe wao kwenye Michuano ya Kombe la Dunia la FIFA 2026 baada ya kufanya kweli dhidi ya Uholanzi ‘The Orange’ katika mtanange mkali uliopigwa dimba la Monterrey, Guadalupe nchini Mexico.
Baada ya dakika 90 za jasho na damu kumalizika kwa sare ya 1-1, Morocco walionyesha umahiri mkubwa kwenye mikwaju ya penalti na kuibuka kidedea kwa shabaha ya 3-2, hatua inayowavusha rasmi kutoka 32 bora hadi 16 bora.
Hatua Inayofuata:
Katika hatua ya 16 bora, Morocco sasa watakutana uso kwa uso na mmoja wa wenyeji wa michuano hii, timu ya taifa ya Canada.
Muhtasari wa Mechi (FT: Uholanzi 1-1 Morocco)
Wafungaji wa Mabao:
-
⚽ 72’ Cody Gakpo (Uholanzi)
-
⚽ 90+1’ Sofiane Diop (Morocco)
Tofauti Ilipoingia (Matokeo ya Penalti):
-
Netherlands 🇳🇱: ✅ ❌ ✅ ❌ ❌ (Walikosa penalti 3)
-
Morocco 🇲🇦: ❌ ✅ ✅ ❌ ✅ (Walipachika penalti 3)
