
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeishushia klabu ya Yanga faini kubwa ya Shilingi milioni 100 kwa kosa la kugomea chumba cha kubadilishia nguo (dressing room) katika mchezo wao dhidi ya JKT Tanzania uliopigwa kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam. Badala yake, Yanga walitumia nyumba iliyopo nje ya uwanja kuvunja kanuni ya 17:20.
Kutokana na kosa hilo kujirudia (baada ya kupigwa faini ya milioni 30 mwezi Mei), Rais wa Yanga, Eng. Hersi Said, na Mtendaji Mkuu (CEO), Andre Mtine, wamepelekwa rasmi Kamati ya Maadili ya TFF kutoa maelezo.
Maamuzi Mengine ya TPLB (Julai 2, 2026):
-
📉 Mtibwa Sugar: Imepigwa faini ya Sh milioni 5 kwa kutotumia chumba cha kuvalia kwenye mechi dhidi ya Namungo FC mkoani Lindi.
-
đź‘• KMC FC: Imepewa onyo kali kwa wachezaji wao watatu kuvaa jezi zenye namba zinazozidi 70, jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
-
❌ Stand FC Masasi yawajibishwa: Wanyang’anywa ushindi wao wa 1-0 dhidi ya Pan African na kupewa Pan African (3-0) kwa kosa la udanganyifu wa usajili. Mchezaji Ramadhani Mlaponi na Kocha Mbano Kizito wote wamefungiwa miezi 12 kila mmoja, huku kocha akipigwa na faini ya Sh 500,000.
