
Kocha wa timu ya taifa ya Senegal, Pape Thiaw, ametangaza kujiuzulu rasmi nafasi yake ya Ukocha wa timu hiyo, siku chache baada ya Senegal kuondolewa katika hatua ya 1/16 ya Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Ubelgiji.
Uamuzi huo umefanyika katika hali ya shinikizo kubwa kwa benchi la ufundi, kufuatia matokeo hayo ambayo yaliwaumiza Mashabiki na Wachezaji.
Kujiuzulu kwa Thiaw kunafungua njia ya mabadiliko makubwa katika benchi la ufundi la timu hiyo, ikiwa ni sehemu ya mpango wa kuijenga upya timu kuelekea mashindano yajayo ya kimataifa.
Wakati huo huo, tayari majina kadhaa yameanza kuhusishwa kuchukua nafasi yake katika kuongoza Simba wa Teranga.
