Mahakama Kuu Yasema Tundu Lissu Ana Kesi ya Kujibu Kwenye Tuhuma za Uhaini

Mahakama Kuu Yasema Tundu Lissu Ana Kesi ya Kujibu Kwenye Tuhuma za Uhaini

Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, leo Agosti 21, 2026 imetoa uamuzi kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, ana kesi ya kujibu katika shauri la uhaini linalomkabili.

Uamuzi huo umesomwa na kiongozi wa jopo la majaji watatu wanaosikiliza kesi hiyo, Jaji Dunstan Ndunguru, ambaye ameeleza kuwa baada ya kupitia ushahidi wa upande wa mashtaka na hoja za utetezi, mahakama imejiridhisha kuwa kuna msingi wa mshtakiwa kujitetea.

Lissu anakabiliwa na shtaka la uhaini kinyume na Kifungu cha 39(2)(d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu (iliyorekebishwa 2023). Mashtaka hayo yanatokana na kauli alizotoa Aprili 3, 2025 Makao Makuu ya CHADEMA, zikihusishwa na nia ya kushawishi umma kuzuia kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Jaji Ndunguru amebainisha kuwa katika hatua hii, jukumu la mahakama lilikuwa ni kuangalia kama ushahidi uliowasilishwa unaweza kumtia hatiani mshtakiwa bila kuingia kwa undani katika kuchambua uaminifu wa ushahidi huo, huku pia ikizingatiwa kuwa Lissu ameshakiri kuwa ni raia wa Tanzania.

Related Posts