
Cristiano Ronaldo amefungua akaunti yake ya magoli kwenye Ligi kuu ya Saudi Pro kwa msimu wa 2026/27 akiifungia Al-Nassr FC bao la nne katika ushindi mnono wa 4-0 dhidi ya Al-Riyadh SC kwenye mchezo wa ligi hiyo uliochezwa leo Agosti 21, 2026.
Ronaldo alianzia benchi kabla ya kuingia mnamo dakika ya 62 akichukua nafasi ya Abdullah Al-Hamdan na kuhitimisha ushindi huo wa Al Nassr FC kwa kufunga bao safi dakika ya 83 akipokea pasi kutoka kwa Ayman Yahya, ikiwa ni bao lake la 977 kwenye maisha yake ya soka akizidi kusogelea rekodi ya kufunga magoli 1000.
FT: Al Riyadh 0-4 Al-Nassr FC
⚽ 18’ Al-Amri
⚽ 45+1’ Ângelo Gabriel
⚽ 58’ João Félix
⚽ 83’ Ronaldo
