Yanga Hawana Huruma Wawabaruza Wanajeshi JKT Tanzania 4-0

Yanga Hawana Huruma Wawabaruza Wanajeshi JKT Tanzania 4-0
Yanga Hawana Huruma Wawabaruza Wanajeshi JKT Tanzania 4-0

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga SC, wameendeleza wimbi la ushindi baada ya kuichapa JKT Tanzania mabao 4-0 katika mchezo uliopigwa Agosti 24, 2026, kwenye Uwanja wa KMC, Mwenge jijini Dar es Salaam.

Yanga walimaliza mpira kipindi cha kwanza baada ya kupata mabao matatu ya haraka kupitia kwa Albert Kangwanda (29′), Ibrahim Bacca (34′), na Chadrack Boka (39′). Kipindi cha pili, mshambuliaji Peter Shalulile alihitimisha Karamu hiyo ya mabao kwa kufunga la nne dakika ya 64. Kangwanda aliibuka Mchezaji Bora wa Mechi (Man of the Match) kufuatia kuhusika kwenye mabao matatu (bao 1 na asisti 2).

Ushindi huo ni wa tatu mtawalia kwa Yanga msimu huu, ukiwafikisha kileleni mwa msimamo wa ligi wakiwa wameweka kimiani jumla ya mabao 11 na kuruhusu mawili pekee.

Related Posts