BREAKING: Emmanuel Nchimbi Afukuzwa Uanachama CCM

BREAKING: Emmanuel Nchimbi Afukuzwa Uanachama CCM
BREAKING: Emmanuel Nchimbi Afukuzwa Uanachama CCM

BREAKING: Emmanuel Nchimbi Afukuzwa Uanachama CCM

Katibu Mkuu wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi, amefukuzwa uanachama wa chama hicho.

Uamuzi huo umetangazwa usiku wa leo Jumatano, Agosti 26, 2026, na Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Asha-Rose Migiro, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi Ndogo za CCM, Lumumba, jijini Dar es Salaam.

ALSO READ | Rais Samia Aridhia Nchimbi Kujiuzulu Umakamu wa Rais wa Tanzania

Dkt. Nchimbi amefukuzwa uanachama siku moja baada ya kumuandikia Rais Samia Suluhu Hassan barua ya kuomba kujiuzulu nafasi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ombi ambalo lilikubaliwa.

Dkt. Migiro amesema uamuzi huo umetokana na maazimio ya vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM vilivyokutana jijini Dar es Salaam kuanzia asubuhi hadi usiku wa leo.

Amesema miongoni mwa ajenda zilizojadiliwa katika vikao hivyo ni suala la maadili lililokuwa likimkabili Dkt. Nchimbi, ambapo vikao vyote vilijadili suala hilo na kufikia uamuzi wa kumfukuza uanachama.

ALSO READ | BREAKING: Nchimbi Atangaza Kujiuzulu Nafasi ya Makamu wa Rais

Related Posts