
CCM Yampendekeza Deogratius Ndejembi Kuwa Makamu wa Rais
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, ametangaza kuwa Halmashauri Kuu ya CCM imempitisha kwa kauli moja Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, kuwa mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
ALSO READ | BREAKING: Emmanuel Nchimbi Afukuzwa Uanachama CCM
Uamuzi huo umefikiwa kufuatia vikao vya chama vilivyoketi jijini Dar es Salaam, ambavyo vimeridhia jina la Ndejembi ili kujaza nafasi hiyo iliyoachwa wazi baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi. Balozi Migiro ameeleza kuwa jina hilo sasa litawasilishwa Bungeni kwa ajili ya hatua za kikatiba za uthibitisho.
ALSO READ | Ukweli Kuhusu Tukio la Ndege Iliyopotea Angani na Kurudi Tena Duniani Baada Ya Miaka 35
