Matusi Yamponza Massanza Apigwa Faini na TFF ya Shilingi Milioni 10

Massanza
Massanza

Matusi Yamponza Massanza Apigwa Faini na TFF ya Shilingi Milioni 10

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), imepitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kutoa maamuzi kadhaa katika kikao chake kilichofanyika Septemba 3, 2026.

Miongoni mwa maamuzi yaliyotolewa ni kumtoza Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Singida Black Stars, Hussein Massanza, faini ya Sh. milioni 10.

Massanza ameadhibiwa kwa kosa la kushutumu na kutumia lugha ya matusi dhidi ya mwamuzi kupitia moja ya machapisho yake kwenye mtandao.

Kwa mujibu wa TPLB, kitendo hicho ni kinyume na Kanuni ya 49:3 na 49:4 ya Ligi Kuu Tanzania, zinazohusu udhibiti na mwenendo wa Maofisa Habari wa Klabu.

Kamati imesisitiza kuwa maofisa wa klabu wanapaswa kuzingatia kanuni na taratibu za mashindano katika matumizi ya majukwaa ya mawasiliano, ikiwemo mitandao ya kijamii.

Related Posts