Taarifa Muhimu Kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Kuhusu Ununuzi wa Luku

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limewataarifu Wateja wake kuwa huduma ya ununuzi wa umeme wa LUKU imerejea katika hali ya kawaida, baada ya awali kukumbwa na changamoto iliyosababisha baadhi ya njia za malipo kushindwa kufanya kazi.

Kupitia ujumbe mfupi wa simu (SMS) uliotumwa kwa Wateja leo, Novemba 17, 2026, saa 3 usiku, TANESCO imesema Wateja wanaweza kuendelea kufanya manunuzi ya umeme kama kawaida, huku ikiwashukuru kwa uvumilivu wao wakati wa changamoto hiyo.

“Ndugu Mteja, tunakutaarifu kuwa huduma ya manunuzi imerejea, sasa unaweza kuendelea kufanya manunuzi, asante kwa uvumilivu wako,” umeeleza ujumbe huo.

Awali, TANESCO ilitangaza kuwepo kwa hitilafu katika Mfumo wa Malipo ya Serikali (GePG), iliyoathiri ununuzi wa umeme kupitia mitandao ya simu na njia za kibenki, na kuwashauri Wateja kutumia Mawakala wa LUKU wakati Wataalamu wakiendelea kushughulikia changamoto hiyo.

Related Posts