Chalamila “Nikifa Nisizikwe Kwa Gharama Kubwa”

 

 

Chalamila "Nikifa Nisizikwe Kwa Gharama Kubwa"
Chalamila “Nikifa Nisizikwe Kwa Gharama Kubwa”

Chalamila “Nikifa Nisizikwe Kwa Gharama Kubwa”

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amefafanua kauli yake aliyowahi kuitoa miezi kadhaa iliyopita kuhusu namna anavyotamani kuzikwa pindi atakapofariki dunia, akisema baadhi ya Watu waliitafsiri vibaya kwa kudhani alimaanisha azikwe kwa taratibu za dini ya Kiislamu.

Akizungumza na AyoTV, Chalamila amesema yeye ni Mkristo Mkatoliki na kwamba alichomaanisha ni kutamani kuzikwa kwa haraka kama wanavyofanya Waislamu, ili kuepusha gharama kubwa za misiba zinazoweza kuziacha Familia katika hali ngumu kiuchumi.

Chalamila ameeleza kuwa msimamo huo ulitokana na tukio la kufiwa na Rafiki yake ambaye msiba wake ulidumu kwa wiki nzima na kutumia fedha nyingi, lakini baada ya maziko, Mtoto wa Marehemu alimtafuta akiomba msaada wa ada ya shule, jambo lililomuumiza na kumfanya kuhoji umuhimu wa kutumia gharama kubwa kwenye maziko huku Watoto wa Marehemu wakiachwa bila msaada.

Amesema jamii inapaswa kubadili mtazamo kuhusu matumizi ya fedha kwenye misiba, akieleza kuwa si busara kutumia mamilioni ya fedha kununua majeneza ya gharama kubwa na kuandaa maziko ya kifahari wakati Marehemu ameacha Watoto wanaohitaji elimu na mahitaji mengine muhimu.

Related Posts