Nature

WAZIRI Silaa Afafanua Suala la Serikali Kuzuia Mitandao Kama X

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa ameeleza kuwa Wizara hiyo itaendelea kuwalinda Watanzania kwa kusimamia maudhui mbalimbali mtandaoni ikiwamo mitandao ya kijamii ili kuhakikisha sheria na taratibu za nchi zinafuatwa.

Silaa amesema hayo katika kipindi maalumu Cafetalk @cafetalk_tanzania kilichofanyika siku ya Jumapili Juni 22, 2025 wakati akijibu maswali ya jopo la wanahabari nguli kuhusu zuio la baadhi ya mitandao ya kijamii kama X kuzuiwa nchini Tanzania.

Ameeleza kuwa baadhi ya maudhui ya baadhi ya mitandao hiyo imekuwa ikikiuka sheria, kanuni, na utaratibu ambao taifa la Tanzania limejiwekea.

“Hauwezi ukaacha mila na desturi za nchi yetu, hauwezi ukaacha maadili ya taifa letu, huwezi sheria za nchi kuvunjwa, hata baa ipo kwa mujibu wa sheria”, ameeleza Silaa.

Related Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *