Afisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe, ametoa kauli zenye kuibua mjadala kuelekea mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2024/2025 dhidi ya watani wao wa jadi, Simba SC. Kamwe amesema Yanga walimfukuza Zanzibar kwa madai kuwa “friji lake ni bovu”, akieleza kuwa haelewi walipofanyia maandalizi wala namna watakavyoingia Dar es Salaam.
“Yanga wamenifukuza Zanzibar kwa sababu wanajua friji langu bovu. Sijui maandalizi watafanyia wapi na sijui wataingiaje Dar es Salaam,” amesema Kamwe kwa kejeli, akimaanisha mazingira ya usiri katika maandalizi ya wapinzani wao.
Hata hivyo, Kamwe amesisitiza kuwa hakuna shaka kwamba timu ya Yanga itakuwepo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Jumatano kwa ajili ya mchezo huo wa kukata na shoka.
Akizungumza kuhusu ugumu wa mchezo dhidi ya Simba SC, Kamwe amesema si jambo rahisi kuwafunga wapinzani wao hao wa jadi, akirejea mchezo wa mwisho kati ya timu hizo mbili ambapo Yanga ilihitaji juhudi kubwa kupata bao la ushindi.
“Si jambo jepesi kushinda mechi dhidi ya Simba SC, maana hata mechi ya mwisho tulihangaika sana kupata goli. Ila watu wajue, si jambo jepesi kuwafunga Simba SC, ni jambo gumu na ndiyo maana tunajipanga sana,” amesema Kamwe.
Kauli hizi zinaibua hamasa zaidi kuelekea mchezo huo wa mwisho utakaobeba hatma ya ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu, huku Yanga wakihitaji sare au ushindi, na Simba wakilazimika kushinda ili kutwaa taji.
Alikataa kuolewa ili amkomboe mama yake... Lakini mama ndiye aliyemuuza!
GORYANAH –Hii ni story ya Moto Sana yenye hisia na Mafunzo, binti jasiri anayepambana na siri nzito, umaskini na hatari kubwa kwa ndoto zake! Pakua app yetu ufurahie Sehemu ya 1 Hadi ya 5,na mwendelezo wake kila JUMAMOSI SAA MOJA KAMILI JIONI BURE!
Ukiona ujumbe wa allow notification bonyeza allow ili uwe mwanafamilia.