Nature
Wafanyabiasha Kwa Njia ya Mtandao Wapewa Mwezi Mmoja Kujiandisha TRA Kulipa Kodi

KUMEKUCHA: Wafanyabiasha Kwa Njia ya Mtandao Wapewa Mwezi Mmoja Kujiandisha TRA Kulipa Kodi

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Yusuph Juma Mwenda, ametoa wito kwa Wafanyabiashara wa mitandaoni ambao hawajajisajili TRA kujisajili biashara zao mara moja ndani ya kipindi cha mwezi mmoja.

Ameyasema hayo wakati akizindua rasmi utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano (MoU) kati ya TRA na Shirika la Kimataifa linashughulika na masuala ya Kodi (IBFD) ambao umefanyika katika Chuo cha Kodi (ITA) Jijini Dar es salaam leo July 24,2025.

Kamishna Mkuu Mwenda amesema wametoa mwezi mmoja kuanzia August Mosi mpaka August 31,2025 Wafanyabiashara wote wanaoendesha shughuli zao mtandaoni wajisajili TRA ili waanze kuchangia katika kulipa Kodi

Amesema watakaoshindwa kutekeleza agizo hilo la kujisajili ndani ya kipindi cha mwezi mmoja watachukuliwa hatua ikiwemo kutozwa faini maana hawajasamehewa kulipa kodi hiyo wakiwemo wale wanaouza vitu mbalimbali mtandaoni bila kulipa kodi kwani wanavunja sheria kwa kutokulipa kodi hiyo.

“Kuanzia August Mosi tutakuwa na kampeni kubwa ya kuhakikisha kila anayefanya biashara ya kupangisha nyumba kupitia mtandao anasajiliwa na kulipa Kodi pamoja na Watu wanaofanya biashara mtandaoni ambao kipato chao kinazidi Sh. 4,000,000 kwa mwaka nao watatakiwa kulipa Kodi na kila mmoja atalipa kutokana na kipato chake”

Related Posts