Nature

Bawacha ya Chadema Yamnyuka Pole Pole “Tuambie Aliyempiga Risasi Tundu Lissu”

Bawacha ya Chadema Yamnyuka Pole Pole “Tuambie Aliyempiga Risasi Tundu Lissu”

Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) Taifa, Sharifa Suleiman, amemshambulia vikali aliyekuwa Katibu Mwenezi wa CCM Taifa na Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, akimtaka kutoa ukweli kuhusu tukio la kupigwa risasi kwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, badala ya ‘kujifanya’ mtetezi wa haki.

ALSO READ | Mpina Ajitokeza Kumtetea Ummy Mwalimu “CCM Wana Sababu Gani Kumfuta Ummy Mwalimu?”

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Sharifa amesema anashangazwa na kauli za hivi karibuni za Polepole zinazokosoa chama tawala na kutetea viongozi wa CHADEMA, ikiwemo kesi inayomkabili Lissu kwa tuhuma za uhaini.

“Ninashangazwa na Humphrey Polepole ambaye mara zote amekuwa akisema ‘tuwakatae wahuni’, leo hii amekuwa akimpenda Tundu Lissu na kujifanya kumtetea. Kama kweli una nia njema na unakiri ulishiriki maamuzi mengi wakati wa Magufuli, basi toka hadharani utuambie nani aliyempiga risasi Lissu,” amesema Sharifa.

Sharifa ameongeza kuwa, Polepole hawezi kudai kuungana na Watanzania wanaopinga dhuluma wakati akiwa sehemu ya waliokuwa wakihujumu CHADEMA kipindi cha nyuma.

“Usitupake mafuta nyuma ya chupa. Tunajua ulishiriki maamuzi makubwa dhidi ya chama chetu. Watanzania wakusamehe? Sawa, lakini kwanza sema ukweli- nani aliyempiga risasi Tundu Lissu. Vinginevyo, tuwapuuze wahuni, tuwakatae wahuni, kwa sababu wahuni bado wako kazini,” amesisitiza.

Humphrey Polepole, ambaye hivi karibuni alijiuzulu nafasi ya Balozi wa Tanzania nchini Malawi na kuvuliwa hadhi ya ubalozi, amekuwa akitoa matamko makali dhidi ya CCM na Serikali, akisisitiza umuhimu wa haki, demokrasia na kutaka kesi ya uhaini dhidi ya Lissu iondolewe

ALSO READ | TLS Kimeomba kikutana na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Dharura

Related Posts