Nature

Watuhumiwa 3 wa Utekaji na Mauaji ya Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Wauawa Wakitaka Kutoroka

Watuhumiwa watatu wa utekaji na mauaji ya mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Ndaki ya Mbeya, Shyrose Mahande, wamefariki dunia baada ya kujeruhiwa kwa risasi walipojaribu kutoroka wakiwa chini ya ulinzi wa polisi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Benjamin Kuzaga, amesema tukio hilo lilitokea wakati jeshi hilo likiendelea na ufuatiliaji kufuatia mauaji ya Shyrose yaliyotokea Septemba 14, 2025.

Amesema mnamo Septemba 24 na 25, polisi walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao watatu waliotajwa kwa majina ya Marwa Nyahega, Edward Kayuni na Websta Mwantebele, lakini walipata majeraha ya risasi baada ya kujaribu kutoroka na baadaye kufariki dunia.

Kamanda Kuzaga ameongeza kuwa, licha ya vifo vya watuhumiwa hao, jeshi la polisi linaendelea na msako wa kuwatafuta wahusika wengine, akiwemo mganga wa kienyeji anayedaiwa kuhusishwa kwa kupelekewa baadhi ya viungo vya marehemu Shyrose, aliyenyongwa na kisha kuchomwa moto.
14h

Related Posts