Msanii chipukizi wa Tanzania, Abigail Chams, ameikosa tuzo ya BET kwenye kipengele cha Msanii Mpya wa Kimataifa, baada ya kutangazwa kuwa Ajuliacosta kutoka Brazil ndiye mshindi wa mwaka huu.

Abigail, aliyewasili Los Angeles na mameneja wake Seven Mosha na Gabrielle Chams, alihamasisha mashabiki kupiga kura kupitia likes na comments mitandaoni, na alionekana kuongoza mwanzoni. Siku tatu kabla ya tuzo hizo, aliachia wimbo mpya “Hold Me”, uliotajwa kama mkakati wa kuvutia mashabiki zaidi.
Licha ya kushindwa, hatua aliyofikia Abigail ni mafanikio makubwa kwa muziki wa Tanzania, na wengi wanaamini ni mwanzo wa safari yake ya kimataifa.